Propellerads

Kiungo wa Yanga amsikitikia Boban.


                                           

Kiungo wa zamani wa Yanga, Akida Makunda, amebainisha kuwa iwapo kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ angezingatia nidhamu ya juu, angekuwa kuwa mchezaji wa
kipekee Simba ambaye angeheshimika na kustaafu soka kama Steven Gerrard wa Liverpool.

Makunda alisema: “Boban akiwa Simba alikuwa ni mchezaji bora, aliheshimika sana lakini pia alikuwa ana jina kubwa, kitu pekee kilichomtia doa ni ukosefu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja.

“Naamini kama leo hii angezingatia nidhamu angemalizia soka lake Simba na kuheshimika. Kwanza alikuwa ni mchezaji ambaye alijitoa kwa Simba na hata hivyo naamini asingewahi kukubali kusajiliwa timu kama Yanga kwasababu ya mapenzi aliyokuwa nayo kwa Simba.

“Boban angeweza kubaki na kuwa kama baba wa timu, nahodha na hata kiranja mkuu kwenye timu hiyo lakini alipoteza bahati hiyo ambayo ingeweza kumpa sifa ya kihistoria kwenye soka la Kitanzania.”

Mwaka 2013, Simba ilipokuwa ikinolewa na Kocha Mfaransa Patrick Liewig, ilimsimamisha Boban na baadaye kuachana naye kutokana na kosa la utovu wa nidhamu.

Baadaye alijiunga Coastal Union ambayo aliichezea kwa msimu mmoja na kuachana nayo. Hivi sasa ni mchezaji wa Friends Rangers ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Kiungo wa Yanga amsikitikia Boban. Kiungo wa Yanga  amsikitikia Boban. Reviewed by Steve on Tuesday, May 26, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.