Propellerads

Neville: Liverpool imepoteza hadhi ya klabu kubwa

                     
                                       

Nahodha wa zamani wa Manchester United, Garry Neville amesema kauli ambayo huenda ikaendeleza ' bifu' lake na Liverpool baada ya kusema
'mabingwa hao mara 18 wa zamani' wamepoteza hadhi ya klabu kubwa na wanakaribia kuanguka kwenye kundi la timu ndogo.
"Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, mastaa wa Liverpool wamekuwa waking'ang'ania kuondoka." anasema, Neville ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya England, Three Lions. Liverpool ilipoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Stoke City baada ya kupokea kipigo cha mabao 6-1, lakini Neville anachukulia kufeli kwa klabu hiyo ya Mersyside kumsainisha mkataba mpya kiungo mshambulizi, Raheem Sterling kama sababu ya Reds kuendelea kufanya vibaya."
"Kama utalinganisha na Manchester United kwa kipindi hicho, utakuta mchezaji aliyeng'ang'ania kuondoka ni Cristiano Ronaldo." aliongeza Neville, " Angalia Liverpool, iliwalazimu wawauze kwa shingo-upande mastaa kama, Michael Owen, Steve McManaman, Luis Suarez na wengineo."
"Anfield ni uwanja ambao una warudisha nyuma kwa sababu klabu nyingine kubwa zimesonga mbele, kuongeza ukubwa wa uwanja au kujenga uwanja mwingine."
Neville: Liverpool imepoteza hadhi ya klabu kubwa Neville: Liverpool imepoteza hadhi ya klabu kubwa Reviewed by Steve on Tuesday, May 26, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.