Propellerads

Van Gaal ataja sababu ya mafanikio ya Man United msimu huu



Meneja wa Manchester United, Louis Van Gaal amesema
kuboreka kwa kiwango cha sasa cha klabu kumetokana na mauzo aliyoyafanya kipindi cha majira ya joto na kujenga upya kikosi chake.

Red Devils wamepanda mpaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo kwa mara ya kwanza tangu kocha huyo aichukue timu kutoka kwa David Moyes mei 2014 baada ya kuwakung'uta Sunderland 3-0 jumamosi hii.

Van Gaal amesisitiza kua maamuzi yake kuwaruhusu  nyota kama Angel Di Maria, Robin Van Persie, na mchezaji aliyekua kwa mkopo- Radame Falcao kuondoka majira ya joto kumechangia sana kupatikana kwa mafanikio.

"Unahitaji bahati, lakini balance ya timu ni bora zaidi kuliko msimu uliopita" aliiambia The Mirror  "Ninazunguka sasa kwa sababu ninaweza. Kwa maoni yangu mwaka jana hatukua na balance. Nimewaruhusu wachezaji kama 20 au 25 hivi kuondoka , kwa hiyo hii ni timu mpya"
Van Gaal ataja sababu ya mafanikio ya Man United msimu huu Van Gaal ataja sababu ya mafanikio ya Man United msimu huu Reviewed by Steve on Monday, September 28, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.