Tambwe akamia kuwatungua Prisons leo, adai ana ukame
Amissi Tambwe yupo fiti na amesema akipata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga dhidi ya Prisons, basi atahakikisha ni lazima afunge bao.
Yanga leo Jumamosi inacheza mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Kombe la FA kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kwa muda mrefu, Tambwe raia wa Burundi alikuwa nje ya uwanja akisumbuliwa na majeraha ya goti, sasa amepona na amefunguka kwamba:
"Nikipangwa keho (leo), nitapambana nifunge japo bao moja."
Tambwe alisema ana hamu ya kuzifumania nyavu kwani ni muda mrefu amekaa bila ya kufunga bao lolote jambo linalomuumiza moyoni.
"Namshukuru Mungu nipo fiti baada ya kupona goti lililonisumbua kwa muda mrefu, endapo nitapata nafasi ya kucheza mechi ya kesho (leo), nitahakikisha napambana vilivyo ili niweze kufunga nitulize roho yangu," alisema Tambwe.
Tambwe akamia kuwatungua Prisons leo, adai ana ukame
Reviewed by Steve
on
Saturday, April 22, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment