Propellerads

Ngoma na Bossou hawatakuwepo kikosi cha Yanga vs Prisons, sababu ni hii




Straika wa Yanga, Mzimbabwe Donald Ngoma na beki wa kati, Vincent Bossou wameondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachovaana na Prisons.

Yanga leo Jumamosi inatarajiwa kucheza na Prisons mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ngoma na Bossou wa Togo, wameondolewa kikosini kutokana na majeraha mbalimbali, wakati Ngoma akiuguza maumivu ya Nyonga, Bossou yeye anauguza goti.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu, amefunguka kwamba Ngoma anaukosa mchezo huo baada ya kujitonesha majeraha hayo kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger wikiendi iliyopita huko Algiers, Algeria.

Bavu alisema, Bossou yeye alipata majeraha kwenye mazoezi ya mwisho kabla ya kuelekea Algeria kurudiana na MC Alger, hali iliyosababisha aondolewe kwenye msafara wa timu hiyo.

"Tutawakosa Ngoma na Bossou katika mechi dhidi ya Prisons hapo kesho (leo), Ngoma ana majeraha ya nyonga na Bossou anaumwa goti, hawa hawatacheza mechi hiyo.

"Bossou tutampeleka hospitali leo (jan) ila Ngoma yeye anaendelea kupata matibabu kwani amejitonesha tu, hivyo kuna uwezekano Jumatatu akaanza mazoezi," alisema Bavu.

Majeruhi mwingine aliyepo kwenye kikosi cha Yanga ni Justin Zulu ambaye anauguza kidonda cha ugokoni.
Ngoma na Bossou hawatakuwepo kikosi cha Yanga vs Prisons, sababu ni hii Ngoma na Bossou hawatakuwepo kikosi cha Yanga vs Prisons, sababu ni hii Reviewed by Steve on Saturday, April 22, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.