Propellerads

Baada ya adhabu, Banda akiri na kuomba msamaha...haya hapa maneno yake



Baada ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfungia mechi mbili beki wa Simba, Abdi Banda ambapo tayari adhabu hiyo ameshaitumikia, beki huyo amesema hatarudia tena kosa hilo.

Aprili 2, mwaka huu, Banda aliingia matatizoni kwa kumpiga ngumi nahodha na beki wa Kagera Sugar, George Kavila kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati timu hizo zikipambana.

Banda alipelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kosa hilo la kumpiga Kavila na kuadhibiwa kwa adhabu ambayo alishaitumikia kwani alisimamishwa kucheza mechi yoyote hadi suala lake litakaposhughulikiwa.

Banda mwenyewe amefunguka: "Namshukuru Mungu suala langu limeisha, nimekoma na kuna kitu nimejifunza maana nilijiona mkosefu kwa kujadiliwa na watu wengi.

"Sitarudia tena kitendo kama kile licha ya mchezo wa soka kuwa na majaribu mengi ambayo yanaweza kukufanya uchukue uamuzi wowote ule, nimejifunza na kuanzia sasa mimi ni mtu mwema.

"Kusimamishwa mechi mbili hakukuniathiri kwa kuwa mimi ni mchezaji mkubwa ila ninachokiangalia hivi sasa ni kuisaidia timu yangu iweze kutwaa ubingwa."

Hata hivyo, kanuni za ligi kuu zinaweka wazi kwamba mchezaji anayepigana au kupiga uwanjani anafungiwa kucheza mechi tatu au zaidi, habari kutoka ndani ya Kamati hiyo zinasema Banda aliomba msamaha.
Baada ya adhabu, Banda akiri na kuomba msamaha...haya hapa maneno yake Baada ya adhabu, Banda akiri na kuomba msamaha...haya hapa maneno yake Reviewed by Steve on Saturday, April 22, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.