Propellerads

Mbrazil Coutinho bado anatamani kurejea Yanga, kwa sasa yupo huku




Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga Mbrazili, Andrey Coutinho ambaye hivi sasa anachezea Nongbua Pitchaya FC ya Thailand, amesema bado ana ndoto za kurejea Jangwani.

Mbrazili huyo aliondoka Yanga kwenye msimu wa 2014/2015 baada ya kusitishiwa mkataba wake kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Mniger, Issofou Boubacar aliyeichezea timu hiyo kwa miezi sita.

Coutinho kabla ya kutua kuichezea Nongbua Pitchaya alikuwa akicheza soka la kulipwa huko Myanmar barani Asia.

Coutinho amefunguka kwamba bado ana mapenzi na klabu yake hiyo ya zamani aliyoichezea kwa mafanikio ya kutwaa taji la ubingwa wa ligi kuu na Ngao ya Jamii, mwaka 2014.

Kiungo huyo amesema angependa kurejea kuichezea Yanga mara baada ya mkataba wake kumalizika lakini siyo hivi sasa huku akiwataja viungo wawili Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko ambao anatamani siku moja acheze nao.

"Nashukuru hivi sasa ninaendelea vizuri na nimeondoka Myanmar nilipokuwa nacheza soka na kuhamia nchini Thailand kwenye Klabu ya Nongbua Pitchaya FC.

"Bado nina mipango ya kurejea kuichezea tena kwa mara ya pili Yanga kama wakinihitaji nitarejea hapo baadaye mkataba wangu ukiwa  umemalizika.

"Ninafurahi maslahi ya huku Thailand ninayoyapata zaidi ya huko nilipokua nacheza awali," alisema Coutinho anayetumia mguu wa kushoto.
Mbrazil Coutinho bado anatamani kurejea Yanga, kwa sasa yupo huku Mbrazil Coutinho bado anatamani kurejea Yanga, kwa sasa yupo huku Reviewed by Steve on Friday, April 21, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.