Kessy ameweka wazi kutolewa na Waarabu kulivyovuruga mipango yake
Beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy ametamka kuwa kitendo cha timu yake kuondolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kumetibua mipango aliyoiweka.
Kessy alitoa kauli hiyo mara tu baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo na MC Alger ya Algeria kwa kufungwa jumla ya mabao 4-1.
Kessy amesema alipanga kutumia michuano hiyo mwaka huu kwa ajili ya kujitangaza kimataifa ili afungue soko.
"Kitendo cha timu yangu ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya kimataifa na Waarabu kimeharibu mipango yangu yote niliyoiweka, kwa kifupi nilipanga kuitumia kwa ajili ya kutengeneza soko kwa kujitangaza kwa kucheza soka la kiwango cha juu.
"Kama unavyojua timu inaposhiriki michuano ya kimataifa, wachezaji mnapata nafasi ya kutazamwa na mawakala wengi wa nchi mbalimbali wanaokuja kutazama mechi zenu.
"Hivyo basi kitendo cha kuondolewa mapema kimenivuruga na kikubwa zaidi nilikuwa nishaaminika kwa makocha na viongozi kunipa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, lakini sitakiwi kukata tamaa ninaamini mwakani tutashiriki tena," alisema Kessy.
Kessy ameweka wazi kutolewa na Waarabu kulivyovuruga mipango yake
Reviewed by Steve
on
Friday, April 21, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment