Prisons wawapiga mkwara Yanga, eti watawavuruga kama Waarabu..stori kamili hapa
Tanzania Prisons imesem itawavuruga Yanga kwa kuwapa kipigo katika mechi ya Kombe la Shirikisho (FA) utakayochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga wataingia uwanjani baada ya kufungwa mabao 4-0 na MC Alger katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyochezwa wiki iliyopita nchini Algeria.
Akizungumza mapema jana, Katibu Mkuu wa Prisons, Osward Morris, alisema wataivuruga Yanga kama walivyovurugiwa na MC Alger.
Morris alisema anajua Yanga watafikiria wanakutana na timu dhaifu ila wajiandae kupambana na watu wanaotaka ushindi.
Alisema anafahamu timu hiyo imevurugwa baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya kimataifa hivyo watataka kumalizia hasira katika mchezo huo.
Morris alisema hali hiyo itaufanya mchezo kuwa mgumu ukizingatia na wao watatamani nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
"Yanga wasije wakajidanganya na kutubeza, tutawaondoa mapema kwenye FA.
Licha ya kuwa soka lina matokeo matatu, lakini mwaka huu tunataka kuonyesha kwamba tuna uwezo wa kufika fainali na mapambano yetu yataanzia kwenye mchezo huo," alisema Morris.
Prisons wawapiga mkwara Yanga, eti watawavuruga kama Waarabu..stori kamili hapa
Reviewed by Steve
on
Thursday, April 20, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment