Omog bado asisitiza nafasi ya Mnyama kuchukua ubingwa, azungumza haya
Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Omog, amewapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kuwa ubingwa wa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara utatua Msimbazi.
Akizungumza mapema jana, Omog alisema ana uhakika wa kufanya vizuri katika mechi tatu zilizosalia za kufunga msimu huo.
Omog ametaka mashabiki wa Simba kutulia kwani bado wana nafasi ya kutwaa ubingwa licha ya wapinzani wao Yanga kupigana kutetea ubingwa wao.
"Malengo yangu ni kutaka kupata matokeo mazuri katika mechi zinazochezwa kwenye uwanja wa nyumbani ili kuongeza pointi," alisema Omog.
Simba imesaliwa na mechi dhidi ya Mwadui, Stand United na African Lyon.
Omog bado asisitiza nafasi ya Mnyama kuchukua ubingwa, azungumza haya
Reviewed by Steve
on
Thursday, April 20, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment