Propellerads

Lwandamina amweka katika rada za Yanga beki wa Azam FC




Wakati Yanga ikiendelea na mbio za kutetea ubingwa wao, tayari kocha mkuu wa timu hiyo, Mzambia, George Lwandamina ameutaka uongozi wa timu hiyo kuhakikisha unamsajili beki wa kushoto wa Azam FC, Gadiel Michael.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, Mzambia huyo tayari ameshakabidhi mapendekezo yake kwa uongozi wa timu hiyo na wachezaji anaowataka kwa ajili ya msimu huo akiwemo beki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia muda wote.

"Kocha ameanza kuangalia namna ya kutengeneza kikosi chake na miongoni mwa wachezaji wa ndani ambao tunalenga kuwasajili ni beki wa kushoto wa Azam, Gadiel na katibu amepewa jukumu la kuongea naye.

"Katibu ametoa maelekezo kwa maskauti kuanza kumfuatilia kwa sababu inasemekana anamaliza mkataba wake na Azam msimu huu, itakuwa faida kwa Yanga maana lengo la Mwalimu ni kumuongezea changamoto Mwinyi Haji kwani kuna uwezekano wa Oscar Joshua kuondoka," alisema mtoa taarifa.

Hata hivyo Gadiel mwenyewe alipotafutwa alisema kwa sasa hawezi kuongea chochote kutokana na kubanwa na mkataba wake hivyo watafutwe viongozi wa timu yake.
Lwandamina amweka katika rada za Yanga beki wa Azam FC Lwandamina amweka katika rada za Yanga beki wa Azam FC Reviewed by Steve on Wednesday, April 19, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.