Propellerads

Sir Alex Ferguson atetea uamuzi wake wa kumteua David Moyes kama mbadala wake



                         
Aliyekua kocha mkongwe wa Man United amedai yeye na klabu
walikua sahihi kumteua David Moyes kama mrithi wake baada ya kustaafu.

Ferguson alistaafu mwaka 2013 baada ya kuifundisha timu hiyo kwa muda wa miaka 27.

Moyes ambaye kabla alikua akiifundisha Everton, alichaguliwa kuwa mrithi wa Fergie lakini alijikuta akidumu Old Trafford kwa miezi nane pekee.

Lakini Ferguson alipokua akiongea katika Documentary iitwayo Secrets of Success inayotarajiwa kurushwa kupitia BBC jumapili hii, amesimamia maamuzi yake.

"Tulijitahidi kulingana na hali tuliyokuwa nayo," alisema mkongwe huyo.

"Tulichagua mtu sahihi.

"Sidhani kabisa kama tulifanya makosa. Nadhani tulichagua mtu sahihi wa mpira.

"Bahati mbaya mambo hayakua kwake David."

Moyes kwa sasa anaifundisha klabu ya La Liga, Real Sociedad.
Sir Alex Ferguson atetea uamuzi wake wa kumteua David Moyes kama mbadala wake Sir Alex Ferguson atetea uamuzi wake wa kumteua David Moyes kama mbadala wake Reviewed by Steve on Tuesday, October 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.