Propellerads

Antony Martial afunguka namna gani Van Gaal alimshawishi kuitema Chelsea kwa ajili ya Man United


                           
Antony Martial ameweka wazi maamuzi yake ya kujiunga na
Man United majira ya joto.

Nyota huyo mwenye miaka 19 alijiunga United kwa pauni mil 36 katika siku ya mwisho kufungwa kwa usajili pamoja na kwamba raisi wa Monaco, Vadim Vasilyev kufichua wiki iliyopita kua kuna klabu nyingine pia iliweka dili la mwishoni.

Kulingana na gazeti la Manchester Evening News, klabu hiyo ni Chelsea ambao wameripotiwa kua walitoa pesa nyingi zaidi ya Man United.

Lakini nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliamua kuingia Old Trafford ambapo amesisitiza kua bosi wake Louis Van Gaal ana mchango mkubwa katika maamuzi yake.

Alipoulizwa kwanini alichagua United, Martial alijibu "Kwa sababu, kwangu ni miongoni mwa klabu tano bora duniani.

"Na najua Van Gaal alinihitaji. Hicho ndicho kilichonishawishi kuchukua maamuzi yangu. Ilikua ni muhimu sana kumuonesha kocha kua anaweza kuniamini."

Aliongeza "Van Gaal alinipigia simu mimi akaongea na mama yangu ambaye alitafsiri. Nilipofika Manchester nikakutana nae, tuliongea kwa kirefu na ilifanyika haraka."
Antony Martial afunguka namna gani Van Gaal alimshawishi kuitema Chelsea kwa ajili ya Man United Antony Martial afunguka namna gani Van Gaal alimshawishi kuitema Chelsea kwa ajili ya Man United Reviewed by Steve on Tuesday, October 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.