Propellerads

Mourinho amesema alitishika sana na siri hii nzito kutoka kwa Ferguson



             
Jose Mourinho amefichua kua Sir Alex Ferguson alimwambia
mipango yake ya kustaafu miezi kadhaa kabla ya kutangaza kwenye vyombo vya habari.

Kocha huyo Mskochi  mwezi May 2013 alitangaza mipango ya kustaafu ifikapo mwishoni mwa msimu wa 2013/14.

Akiongea katika Documentary ijayo ya BBC inayoitwa 'Sir Alex Ferguson: Secrets of Success' , Mourinho amesema kua alitishika na pale Ferguson alipompa habari hizo.

"Aliniambia siri nzito, watu wengi hawajui, kama mwezi mmoja au miwili kabla, maamuzi yanaweza kua...yanaweza kua kuacha," alisema "Najua aliniamini, kwa sababu kama asingekua hivyo asingeniambia lakini nilitishika.

"Nilitishika mwisho aliviambia vyombo vya habari kuhusiana na maamuzi yake."

Baada ya Ferguson kuondoka na kuwasili David Moyes, Mourinho amesisitiza kua kamwe hakushawishika kuchukua kazi ya United, badala yake alijiandaa kurejea Chelsea.

"Kila meneja ulimwenguni anaiangalia Man United kama klabu kubwa lakini nilitaka kuja Chelsea," aliongeza.




Mourinho amesema alitishika sana na siri hii nzito kutoka kwa Ferguson Mourinho amesema alitishika sana na siri hii nzito kutoka kwa Ferguson Reviewed by Steve on Tuesday, October 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.