Propellerads

Manchester United na Bayern Munich wanachuana kumnasa chipukizi huyu wa zamani wa Everton


                        Shkodran Mustafi
Bayern Munich wameungana na Man United kwenye kinyang'anyiro
cha kumnasa beki wa Valencia, Shkodran Mustafi, hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.

Mustafi alipata kucheza mechi moja ya michuano mikubwa kwa miaka mitatu aliyokua Everton ambapo aliingia badala ya Tony Hibbert dakika ya 75 kwenye mechi ya Europa waliyopoteza dhidi ya BATE Borisov mwaka 2009 kabla hajaruhusiwa kwenda Sampdoria mwaka 2012.

Hata hivyo Mustafi tangu aondoke Everton ameibukia kua miongoni mwa mabeki wanaochukuliwa kuwa na viwango vya juu katika mpira wa Ulaya.

Barcelona, Manchester United na Real Madrid walihusishwa kumtaka beki huyo majira ya joto lakini Valencia hawakutaka kumwachia.

Hata hivyo, AS wameripoti kua Bayern Munich nao wameonesha nia ya kumtaka mkali na huenda wakaangalia uwezekano mwezi januari.

Pep Guardiola anadaiwa kumkubali sana nyota huyo ambaye ni raia wa Ujerumani na anaamini anaweza kushawishika kujiunga Bayern Munich.
Manchester United na Bayern Munich wanachuana kumnasa chipukizi huyu wa zamani wa Everton Manchester United na Bayern Munich wanachuana kumnasa chipukizi huyu wa zamani wa Everton Reviewed by Steve on Tuesday, October 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.