Propellerads

Hivi ndivyo Rafa Benitez alivyojibu kauli ya Benzema



                          Default
Meneja wa Real Madrid, Karim Benzema amejibu Kauli ya
mshambuliaji wake Karim Benzema kua amechoka kutolewa mara kwa mara.

Nyota huyo Mfaransa alisema kua maechoka baada ya kutolewa kwenye mechi ya jumapili iliyopita dhidi ya Atletico Madrid.

Sasa Benitez amejibu kile ambacho Benzema alikitamka kwenye vyombo vya habari, ambapo amedai anaelewa malalamiko ya mshambuliaji wake.

"Maneno ya Benzema hayawezi kunikera. Nampenda Karim ,ni balaa sana," aliiambia COPE.

"Hata mimi ningekasirika, kama naweza kufunga halafu meneja anaamua kunitoa."

Katika mechi zote za ligi msimu huu Benzema amepata kucheza, lakini amekamilisha dakika 90 katika mechi moja tu ambayo pia ndio ambayo hakufanikiwa kufunga.

Mfaransa huyo pia alicheza muda wote mechi ya kwanza ya UEFA kwa msimu huu dhidi ya Shakhtar Donetsk lakini alicheza dakika 67 pekee dhidi ya Malmo.

Benzema amefunga magoli saba katika mechi nane katika michuano yote msimu huu.
Hivi ndivyo Rafa Benitez alivyojibu kauli ya Benzema Hivi ndivyo Rafa Benitez alivyojibu kauli ya Benzema Reviewed by Steve on Tuesday, October 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.