Propellerads

Ile kesi ya Messi juu ya kukwepa kodi, mahakama yaamua kutoa hukumu ambayo itakua pigo kwa familia ya Messi



                            
Mwendesha mashitaka nchini Hispania amependekeza
adhabu ya miezi 18 jela na faini zaidi ya  £1.5million kwa baba yake Lionel Messi aitwaye Jorge kwa makosa ya kukwepa kulipa kodi.

Mwendesha mashitaka huyo aliamua kumtoa Messi katika kesi hiyo ya kukwepa kiasi cha £3.1m katika kipindi cha mwaka 2007-09 kwa sababu baba yake Messi ndiye aliyehusika na maswala ya fedha.

Hata hivyo, mahakama iliamua kukataliwa rufaa ya Messi mwaka jana na ilitoa mwongozo kwamba angeweza kupitishwa uundwaji wa mtandao wa makampuni ya kuuza mafuta ambayo yalionekana kutumika kwa kukwepa kodi kutokana na mapato kupitia kivuli chake.

Kodi ilikua ikifichwa kupitia mlolongo wa makampuni ya mafuta Uruguay, Belize, Switzerland  na United Kingdom, kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka.

Messi na baba ake walilipa £3.7m  kwenye mamlaka za kodi kama malipo sahihi baada ya kufunguliwa mashtaka June 2013.

Lionel Messi amekua mkazi wa Barcelona tangu mwaka 2000 na alipata uraia wa Hispania mwaka 2005. Yupo namba 10 katika orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaoingiza pesa nyingi zaidi ulimwenguni katika muongo uliopita.
Ile kesi ya Messi juu ya kukwepa kodi, mahakama yaamua kutoa hukumu ambayo itakua pigo kwa familia ya Messi Ile kesi ya Messi juu ya kukwepa kodi, mahakama yaamua kutoa hukumu ambayo itakua pigo  kwa familia ya Messi  Reviewed by Steve on Wednesday, October 07, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.