Kocha mpya wa Liverpool kutangazwa kabla ya mechi ya Tottenham, hawa wanapewa nafasi kubwa
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Sky News, Klabu ya Liverpool bado
wanangoja kumtangaza kocha wao mpya lakini watafanya hayo kabla ya mechi na Tottenham tarehe 17 Oktoba mwaka huu.
Brendan Rodger amefukuzwa klabuni hapo baada ya kudumu tangu 2012 akitokea Swansea City, na alipigiwa tu simu ya kuondoka kwake baada ya kupata sare na mahasimu wao Everton jana.
Pressure kwa kocha huyo ilianza baada ya kiwango kibovu cha Liverpool msimu huu ambapo wameshinda mechi moja pekee kati ya sita zilizopita. Huku wakishika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi.
Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp na yule aliyekua wa Real Madrid Carlo Ancelotti wanatajwa kua huenda mmoja wao akashika usukani klabu ya Merseyside.
Kocha mpya wa Liverpool kutangazwa kabla ya mechi ya Tottenham, hawa wanapewa nafasi kubwa
Reviewed by Steve
on
Monday, October 05, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment