Bosi wa Man United asisitiza kua 'alistaajabishwa' na kipigo cha Arsenal
Louis Van Gaal amefunguka kua 'alistaajabu' timu yake
Manchester United ikipokea kipigo cha 3-0 kutoka kwa Arsenal jana.
United walishuhudia kwa huzuni magoli matatu yakiingia mapema tu ndani ya dakika 20 baada ya kuanza kwa mchezo kwenye uwanja wa Emirates ambapo Alexis Sanchez alitupia mawili huku akimtengenezea Mesut Ozil goli la tatu.
United hawakuweza kurudisha goli lolote ambapo huu ukiwa ni mchezo wa pili kupoteza msimu huu, na sasa wamejikuta wakiangukia nafasi ya tatu.
Kocha Mholanzi akafunguka "Sikutegemea hivyo. Hatukucheza mchezo wetu tulivyopanga, hatukua na hali ya kushinda.
"Tumepoteza, na tumepoteza katika namna ambayo huwezi kupoteza ukiwa kileleni mwa ligi. Huwezi kuanza kama tulivyoanza, na wanajua hilo."
Kuhusu viungo wake Bastian Schwensteiger na Michael Carrick, Van Gaal amesema "Hakukua na bahati na mpira, hatukua taratibu lakini hatukua wachokozi. Wachezaji kama Carrick na Schwensteiger walikua na nafasi nzuri, lakini unahitaji kua mchokozi na unatakiwa kuutawala mpira.
"Unatakiwa kufanya hivyo sio tu na wawili kwenye kiungo,ni timu nzima. Unahitaji kuchokoza unapokua unapambana, na Arsenal walituchokoza zaidi.
"Unapoipa nafasi kubwa timu kama Arsenal kucheza mpira wao halafu unajua tu utapoteza. Tulijiandaa kua pamoja sana na kutoacha kuleta uchokozi, kwa hiyo sikutarajia kabisa.
"Sijui nini kilitokea. Nilijiuliza zaidi kipindi cha pili na baada ya mechi kwa sababu kawaida ninasema vitu jinsi ninavyoviona. Lakini ni vigumu kujibu kwa wachezaji kwa sababu wote walikua katika wakati mgumu.
"Tatizo halikuanzia nyuma, lilianzia kwenye kiungo. Wachezaji wao wa kiungo haswa Santi Cazorla na Ozil walikua na muda mwingi na nafasi. Na walikua na uwezo wa kutumia nafasi kutoka pale."
Bosi wa Man United asisitiza kua 'alistaajabishwa' na kipigo cha Arsenal
Reviewed by Steve
on
Monday, October 05, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment