Maoni ya Wenger baada ya kutimuliwa kwa kocha Brendan Rodgers wa Liverpool
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema anatarajia kumuona
Brendan Rodgers akifundisha soka tena baada ya kocha huyo kutimuliwa ndani ya klabu ya Liverpool siku ya Jumapili baada ya sare ya kufungana goli 1-1 na mahasimu wao Everton.
Wenger amesema, Rodgers ameonesha anauwezo wa kufundisha kwa uwezo wa juu na kuongeza kuwa amesikitishwa kumuona akiondoka Anfield.
Akizungumza muda mfupi baada ya Liverpool kutangaza kumtimua Rodgers, Wenger alisema: “Najisikia vibaya kila naposikia kocha kafukuzwa kwasababu nadhani Rodgers ni kocha bora”.
“Nadhani hakuwa na bahati ya kutwaa taji la EPL. Alikaribia kufanya hivyo ili aweke historia kati ya makocha waliowahi kuifundisha Liverpool”.
“Lakini hivyo ndivyo ilivyo, namtakia kila laheri. Nina hakika atatafuta kazi sehemu nyingine tena”.
Maoni ya Wenger baada ya kutimuliwa kwa kocha Brendan Rodgers wa Liverpool
Reviewed by Steve
on
Monday, October 05, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment