Propellerads

Victor Valdes azuiwa mazoezini Man United!!





Kwa mujibu wa ripoti inadaiwa kua mlinda mlango wa Man United,
Victor Valdes amekatazwa kuonekana eneo la mazoezi.

Gazeti la The Mirror limedai kua kocha Louis Van Gaal amemwambia kipa huyo kua anaweza kusogea eneo la mazoezi endapo tu kikosi cha kwanza hakipo mazoezini kwa hiyo anaweza  kufanya mazoezi na makocha wa vijana.

Valdes mwenye miaka 33 amekua akihusishwa kutaka kuhamia vilabu vya Chelsea na Liverpool wiki  iliyopita.

Kipa huyo wa zamani wa Barca alisaini United msimu uliopita kama chaguo la pili baada ya David De Gea ,lakini msimu huu amejikuta akiwa nyuma ya De Gea, Sergio Romero na Sam Johnstone.


Victor Valdes azuiwa mazoezini Man United!! Victor Valdes azuiwa mazoezini Man United!! Reviewed by Steve on Tuesday, September 29, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.