Propellerads

Wenger: Cech anaweza kukosa mechi ya Olympiacos




Arsene Wenger amesema anaweza kumuanzisha David Ospina badala ya
Petr Cech kwenye mechi ya klabu dhidi ya Olympiacos leo jumanne.

Ospina alianza kwenye mechi ya kwanza ya Arsenal klabu bingwa msimu huu ambapo walipoteza kwa 2-1 mbele ya Dinamo Zagreb.

"Kitu ninachotaka kusema, sio kwa sababu nimeamua Ospina awe anacheza klabu bingwa. Niataangalia mchezo hadi mchezo na kutakua na maamuzi tofauti." Wenger aliwaambia waandishi.

"Ninahitaji kumpa (Ospina) michezo nadhani ni goli kipa wa kiwango cha juu, lakini haimaanishi kua atacheza.

"Hiyo ni kazi yetu, kazi yetu ni kuchagua na kushindana na wachezaji wengine . Nadhani anafanya vizuri zaidi."

The Gunners wanaweza kupanda hadi nafasi ya pili katika kundi F kama wakiwafunga Olympiacos leo.
Wenger: Cech anaweza kukosa mechi ya Olympiacos Wenger: Cech anaweza kukosa mechi ya Olympiacos Reviewed by Steve on Tuesday, September 29, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.