Paris Saint-Germain wanamtaka Mourinho?
Paris Saint-Germain wanadaiwa kuvutiwa na
Jose Mourinho kama kocha ajaye katika klabu hiyo na wana mpango wa kumnasa msimu ujao.
Kocha huyo mreno amejikuta katika wakati mgumu msimu huu baada ya kua na mwanzo mbovu katika Premier league kwani amepoteza mechi tatu kati ya sita.
Kwa mujibu wa The Express, wakali wa Ligue 1 wanaamini wataweza kumshawishi Mourinho kujiunga nao msimu ujao japokua mkataba wake wa sasa na Chelsea unaisha mwaka 2019.
Kocha wa sasa wa PSG, Laurent Blanc anaonekana kua na uwezo usioridhisha kuipa klabu vikombe hasa klabu bingwa.
Paris Saint-Germain wanamtaka Mourinho?
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 20, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 20, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment