Hakuna kipingamizi kwa Ngoma au Tambwe kuondoka Yanga, mipango 'mahsusi' yawekwa kwa ajili ya kikosi
Yanga wameonyesha kutotaka masihara baada ya kuwatamkia wazi washambuliaji wao wawili, Donald Ngoma na Amissi Tambwe kwamba milango iko wazi wanaweza kuondoka kama wanataka.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Paulo Malume amefunguka kwamba hawatakuwa na kipingamizi kwa nyota yeyote ambaye ataona hafurahishwi na maisha ya Jangwani na kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo.
"Kumekuwapo na tetesi nyingi juu ya kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wetu huku wengine wakiwa wamebakisha miezi michache kabla ya mikataba yao kwisha, tunasema ruksa wao kuondoka, hatuwezi kuwazuia wala kuwazibia riziki zao sehemu nyingine," alisema Malume.
Pia aliongeza kwamba wapo katika mikakati kabambe ya kufanya usajili bab kubwa, baada ya kubaini mapungufu kadhaa katika kikosi chao msimu huu.
"Tutaangalia mshambuliaji mwingine ambaye atakuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote uwanjani baada ya kupata ripoti ya kocha msimu ukimalizika.
"Yanga tuwe watulivu, pesa ipo na tutasajili mchezaji yeyote tunayemtaka, kwa hiyo tutulie japo tumefanya vibaya Ligi ya Mabingwa Afrika tunajipanga kwa Kombe la Shirikisho," alisisitiza.
Hakuna kipingamizi kwa Ngoma au Tambwe kuondoka Yanga, mipango 'mahsusi' yawekwa kwa ajili ya kikosi
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 23, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment