Abdi Banda adaiwa kutosa mkataba mpya Msimbazi, ishu kamili ipo namna hii..
Akiwa amebakisha mechi sita za Ligi kuu Bara sawa na dakika 540 za kuichezea Simba, beki kiraka Abdi Banda amegomea saini ya miaka miwili ya kuichezea timu hiyo.
Banda alitua kuichezea Simba msimu wa 2014/2015 kipindi hicho akiwa anaichezea klabu ya timu ya vijana ya U 20 (Ngorongoro Heroes) na Coastal Union.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwenye kamati ya Utendaji ya timu hiyo, viongozi tayari wamemuandalia na kumpa mkataba baada ya mazungumzo ya awali kufanyika lakini baadaye aligoma kusaini.
Mtoa taarifa alisema beki huyo amegoma kusaini mkataba wa miaka miwili aliyopewa na viongozi wa klabu huku yeye akitaka mwaka mmoja wa kuendelea kukipiga Simba.
"Uongozi hivi sasa upo katika jitihada za kuhakikisha tunawasajili wachezaji wote ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu lakini kwa vigezo maalumu na kikubwa kikiwa ni kiwango na msaada anaoutoa kwenye timu," alisema mtoa taarifa huyo.
Banda mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo, alifunguka haya:
"Nisingependa kulizungumzia hilo kwa sasa hivi kwani ninaogopa kujichanganya hivyo tusubirie mechi hizi sita nilizobakiza zimalizike za ligi kuu ndiyo nitakuwa kwenye sehemu nzuri ya kuongea.
"Naomba niishie hapo na kuhusu kitu kingine chochote kinachohusiana na mkataba, basi aulizwe meneja wangu ataweza kuweka wazi kila kitu."
Abdi Banda adaiwa kutosa mkataba mpya Msimbazi, ishu kamili ipo namna hii..
Reviewed by Steve
on
Friday, March 24, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment