Propellerads

Dida aeleza mkataba na Yanga unavyomzuia kwenda Ulaya




Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi 'Dida' amesema anashindwa kwenda kucheza soka ya kulipwa katika klabu nyingine za Afrika na Ulaya kutokana na mkataba wake unaombana kuondoka Jangwani.

Dida amefunguka kwamba amekuwa akipata ofa nyingi, lakini anashindwa kuondoka kutokana na kufungwa na mkataba aliosaini na klabu hiyo.

Amesema si kwamba hana mipango ya kwenda kujaribu maisha katika klabu nyingine nje ya Tanzania, lakini mkataba unambana kuondoka kwani kulingana na utaratibu uliopo kwenye timu yake, ni ngumu mchezaji mwenye mkataba mrefu kupata nafasi ya kwenda sehemu nyingine hata kama atakuwa amepata ofa nono.

"Nimepata ofa nyingi kwenda kucheza nje, lakini kikwazo ni mkataba nilionao Yanga, hivyo nasubiri umalizike," alisema Dida, hata hivyo hakuweka wazi endapo ataongeza mkataba wake na Yanga au la pindi ukimalizika.
Dida aeleza mkataba na Yanga unavyomzuia kwenda Ulaya Dida aeleza mkataba na Yanga unavyomzuia kwenda Ulaya Reviewed by Steve on Friday, March 24, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.