Unataka kujua hali ya Mwanjali!?, Daktari wa Simba afungukia maendeleo yake hapa
Beki wa Simba raia wa Zimbabwe, Method Mwanjali, ameanza kurejea uwanjani mdogo mdogo, baada ya kuanza mazoezi maalumu kujiandaa na mechi zilizosalia za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mwanjali aliumia goti katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Prisons, uliochezwa Februari 11 mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na sasa daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema beki huyo ameanza mazoezi mepesi.
Gembe alisema kwa sasa amepewa programu maalumu ya mazoezi ya viungo 'gym' kwa muda wa wiki mbili.
Alisema tayari amemaliza siku saba za kwanza bado nyingine saba na akimaliza atarudi hospitali kwa uchunguzi kabla ya kuanza mazoezi na wenzake.
Unataka kujua hali ya Mwanjali!?, Daktari wa Simba afungukia maendeleo yake hapa
Reviewed by Steve
on
Friday, March 24, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment