Simba wajitapa kuwazidi Yanga na Azam 'maujanja' kimataifa!!
Yanga na Simba wanalia hujuma walizofanyiwa wakiwa ugenini kwenye michuano ya kimataifa, lakini Simba wameibuka na kusema wao ni kiboko yao.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu', alisema wanazijua fitina zinazofanywa na wapinzani wao wanapokuwa wanashiriki michuano ya kimataifa.
Kaburu alisema wao ni wazoefu wa kupangua hujuma mbalimbali zinazofanywa na wapinzani wakiwa ugenini tofauti na Yanga na Azam.
Alisema katika msimu wa 2003, waliweza kupangua hujuma walipokuwa ugenini kucheza michuano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zamalek ya Misri na kufanikiwa kuitoa kwao na kutinga robo fainali.
Kaburu alisema waliweza kufanya hivyo katika msimu wa 2011/12 walipocheza na Setif ya Algeria katika michuano hiyo ya kimataifa na kuwaondoa nchini kwao.
Simba wajitapa kuwazidi Yanga na Azam 'maujanja' kimataifa!!
Reviewed by Steve
on
Friday, March 24, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment