Mpaka sasa hiki ndicho kitu pekee kinachomkwamisha Niyonzima kutimkia ughaibuni kwa ajili ya majaribio, mwenyewe aweka wazi kila kitu
Imefahamika kuwa, mechi ya ligi ya Mabingwa Afrika itakayowakutanisha
Yanga na Zanaco ya Zambia imevuruga usajili wa kiungo mchezeshaji wa Wanajangwani Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.
Timu hizo, zinatarajiwa kujitupa leo kwenye uwanja Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa.
Niyonzima amefunguka kwamba mengi yamezushwa juu yake, lakini ukweli ni kwamba alirejea nyumbani kwao kwa ajili ya kuifanyia marekebisho hati ya kusafiria 'passport'.
Ameweka wazi alirejea kuchukua hati hiyo nyumbani kwao Rwanda baada ya kupata ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Cyprus.
Aliongeza kuwa, amepanga kuelekea Cyprus mara baada ya mechi zote mbili ya hapa nyumbani na ugenini zitakapomalizika dhidi ya Zanaco, hivyo ameiomba klabu hiyo inayomhitaji kumsogezea mbele tarehe aliyopangwa kwa ajili ya majaribio.
"Nilitakiwa hivi sasa niwepo nchini Cyprus kwenye moja ya klabu, lakini mechi hii ya Zanaco imenivurugia, hivyo nimepanga kuzungumza na klabu hiyo leo (jana) kwa ajili ya kusogeza mbele tarehe niliyopangiwa kwa ajili ya majaribio.
"Ninatakiwa kuanza kufanya majaribio Machi 14 mwaka huu ambayo ni wiki ijayo tukijiandaa na safari ya Zambia katika mchezo wa marudiano, hivyo utaona jinsi gani ratiba itakavyokua imenibana.
"Ni vyema ikafahamika hivyo, lakini kiukweli mimi sikuwa na tatizo lolote kutoka kwa viongozi au shabiki kwa sababu mengi yalizungumzwa nilivyorudi nyumbani Rwanda kushughulikia matatizo yangu ya pasipoti," alisema Niyonzima.
Mpaka sasa hiki ndicho kitu pekee kinachomkwamisha Niyonzima kutimkia ughaibuni kwa ajili ya majaribio, mwenyewe aweka wazi kila kitu
Reviewed by Steve
on
Saturday, March 11, 2017
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, March 11, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment