Propellerads

Mwaka huu mbona watamkoma Ngoma wa Yanga!!, ona anavyotamba




Tayari ana mabao mawili katika Ligi Kuu Bara aliyoyapata katika
mechi mbili, straika wa Yanga, Donald Ngoma amesema ataendelea kufunga katika kila mechi labda aumie.

Ngoma ameifungia Yanga bao moja katika mchezo dhidi ya Coastal Union ambao washinda mabao 2-0, pia akafunga moja dhidi ya Prisons ambapo walishinda mabao 3-0.

Katika orodha ya ufungaji bora, Ngoma anaongoza kwa mabao yake mawili akiwa sawa na Hamis Kiiza wa Simba, Atupele Green (Ndanda FC) na Miraji Athuman wa Toto Africans.

Ngoma alisema ana mipango mingi ya kuifanyia Yanga lakini kwa sasa lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaiongoza kushinda katika kila mechi.

“Nitajitahidi kufunga katika kila mechi kama nilivyoanza, labda itokee nimeumia au matatizo mengine ya kimchezo, nafanya mazoezi kwa bidii ili nifunge na kuipatia Yanga ushindi.
“Hata kama sitafunga mimi basi nataka kuwa natoa pasi za kufunga ambazo wenzangu watazitumia vizuri kupata ushindi, hapa nataka Yanga itetee ubingwa wake si vinginevyo,” alisema Ngoma, raia wa Zimbabwe.

“Nawaomba wachezaji wangu tuendelee kushirikiana na tuachane na ubinafsi, tukifanya hivyo mambo yatakuwa mazuri kwetu katika kila mechi na hakuna timu itakayotusumbua.”
Mwaka huu mbona watamkoma Ngoma wa Yanga!!, ona anavyotamba Mwaka huu mbona watamkoma Ngoma wa Yanga!!, ona anavyotamba Reviewed by Steve on Saturday, September 19, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.