Ngoma kuikosa mechi ya marudiano Zambia, majeraha yamemkalisha nje kwa wiki moja, daktari ameeleza zaidi...
Pamoja na mbio za klabu ya Yanga kwenda kusaka ushindi wa namna yoyote nchini Zambia dhidi ya Zanaco FC, timu hiyo imefikwa na shaka kutokana na mshambuliaji wao raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma kutokuwa fiti tena kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo wao wa kwanza wa timu hizo Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Katika mchezo huo ambapo ulimalizika kwa sare ya 1-1, Ngoma alicheza kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza na kutolewa kutokana na kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Emmanuel Martin.
Daktari wa Yanga, Edward Bavu amesema Ngoma alitoneshwa kwenye goti lake jambo ambalo liliwafanya siku hiyohiyo walianza kumpatia matibabu, ambayo ameendelea nayo tangu jana, lakini jambo la uhakika atakuwa nje wiki moja.
"Ngoma hatakwenda Zambia kwenye mchezo wa marudiano kwa kuwa bado anaumwa, ni pengo kubwa hasa ukizingatia mchezo huo tunahitaji ushindi wa aina yoyote ili tuweze kuendelea kwenye michuano hiyo.
"Kwa kushirikiana na madaktari wenzangu, tunaendelea kumpatia tiba lakini hataweza kuungana na wenzake kwani atatakiwa kufanya mazoezi ya pekee zaidi ili aweze kuimarika vizuri, naamini ndani ya siku tatu hadi hadi wiki atakuwa yuko fiti kiasi cha kurejea kwenye ubora wake, hivyo timu itamkosa mchezo huo tu lakini ijayo atakua safi," alisema Bavu.
Ngoma kuikosa mechi ya marudiano Zambia, majeraha yamemkalisha nje kwa wiki moja, daktari ameeleza zaidi...
Reviewed by Steve
on
Wednesday, March 15, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment