Propellerads

Kuhusu ishu ya kuwasajili Ngoma na Msuva, Hanspoppe afafanua nje ndani ya mchongo ulivyo



Baada ya habari za muda mrefu kwamba vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba wana mpango wa kuwasajili wachezaji wawili nyota wa Yanga, Simon Msuva na Donald Ngoma, hatimaye mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amevunja ukimya.

Hans Poppe amesema suala la kuwasajili Ngoma na Msuva linawezekana kabisa kwao lakini ni swala la muda tu kwa kuwa wako tayari kuwasajili hasa ikibidi kuwa hivyo.

"Kwa sasa hatujazungumza nao, pia kikosi chetu kipo kamili lakini kwa mfano angalia sasa tunapambana kubeba ubingwa. Tukifanikiwa maana yake tunaingia kwenye ligi ya Mabingwa Afrika. Hii si michuano rahisi.

"Lazima tutajiimarisha na wachezaji kama Ngoma na Msuva ni muhimu. Msuva tupo tayari kumsajili wakati wowote na nilishaeleza tangu mwanzo kuhusiana na hilo," alisema Hans Pope.

"Kweli kabisa Msuva ni mchezaji mzuri, sema ana bahati mbaya anacheza timu ambayo watu hawamuelewi wala hawaoni anachokifanya.

"Kuhusu Ngoma, hakika ni mchezaji mzuri kabisa. Ukiniambia nichague Ngoma au Tambwe, basi moja kwa moja naenda kwa Ngoma.

"Kwake kikubwa ambacho tutaangalia ni suala la majeraha kama ambavyo unaona sasa. Kama yuko fiti, bsi tunamchukua, ukimuunganisha na kina Ajibu, Mavugo, Kichuya, Mo, Ibrahi itakuwa si mchezo," aliongeza Hans Poppe akionyesha kujiamini kabisa.

Kuhusu ishu ya kuwasajili Ngoma na Msuva, Hanspoppe afafanua nje ndani ya mchongo ulivyo Kuhusu ishu ya kuwasajili Ngoma na Msuva, Hanspoppe afafanua nje ndani ya mchongo ulivyo Reviewed by Steve on Wednesday, March 15, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.