Yanga wagonga hodi Azam FC, wanamtaka mrithi wa Haji Mwinyi
Yanga wameanza mkakati wa kumnasa beki wa nguvu wa Azam FC, Gadiel Michael. Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinadai kwamba mmoja wa vigogo wa klabu hiyo ameanza mchakato wa kutafuta njia ya mawasiliano ya kinda huyo kutoka kwa watu wake wa karibu na kuna uwezekano mkubwa mambo yakamalizika mapema.
"Kama ukiiangalia timu yetu utagundua kuwa nafasi ya beki wa kushoto ina matatizo kidogo na kwa kuligundua hilo, kuna mikakati mizito ya kumsajili beki wa Azam FC, Gadiel Michael.
"Ni kweli tunaye Oscar Joshua pamoja na Hajji Mwinyi, lakini wanaonekana kuwa na madhaifu flani hivyo tumeamua kufanya mchakato wa kuongeza mtu ambaye atawapa changamoto," alisema kigogo mmoja wa Yanga.
Gadiel Michael |
Kigogo huyo alisema amefanya mawasiliano na mmoja wa watu wanaomsimamia mchezaji huyo lakini akashauri kuwa avute subira kidogo kwani kila kitu kitakwenda sawa, ikizingatiwa kuwa beki huyo amebakisha miezi sita kwenye mkataba wake na Wanalambalamba hao.
Gadiel mwenyewe alipotafutwa amefunguka haya,
"Bado nina mkataba na Azam, kama kweli Yanga wanahitaji basi wasubiri nimalize mkataba wangu au kufanya mazungumzo na mabosi wangu, vinginevyo kwa sasa akili yangu inalenga kuipigania timu ili kufanya vizuri katika mashindano yote inayoshiriki," alisema.
Yanga wagonga hodi Azam FC, wanamtaka mrithi wa Haji Mwinyi
Reviewed by Steve
on
Wednesday, March 15, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment