Propellerads

Simba ndani ya hesabu kali za kumnasa kiungo wa Zanaco



Simba wana ndoto kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu na kama wakifanikiwa, watashiriki michuano ya kimataifa na sasa wameamua kuwahi katika suala la kusaka wachezaji wazuri na wenye uzoefu mkubwa, wakiwa wamelenga kumnasa kiungo Rasta wa Zanaco, Zimeseleni Moyo aliyewasumbua Yanga.

Vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara walikuwa makini kuangalia viwango vya wachezaji wa Zanaco walipokuwa wakicheza na Yanga mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na wakaondoka na jina moja la Zimeseleni Moyo 'Rasta'.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinadai kuwa baadhi ya viongozi walishuhudia mchezo huo dhidi ya Yanga na Zanaco na kuridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo na sasa wanaandaa mpango mkakati wa kuinasa saini yake.

"Haya mambo yanakwenda kwa siri sana kwani tunapotangaza kuwa kuna mchezaji tunayemsajili, wenzetu (Yanga) wanatuzunguka mlango wa nyuma na sasa tumeamua kumfuatilia kimyakimya," alisema kigogo mmoja.
Simba ndani ya hesabu kali za kumnasa kiungo wa Zanaco Simba ndani ya hesabu kali za kumnasa kiungo wa Zanaco Reviewed by Steve on Wednesday, March 15, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.