Propellerads

Ronaldo ampigia debe Mreno mwenzake Real Madrid, Chelsea bado wanamtaka Lukaku, hizi hapa stori za usajili magazeti ya Ulaya leo



Imeripotiwa kwamba Cristiano Ronaldo ameiomba klabu yake ya Real Madrid kumsaini Mchezaji mwenzake katika timu ya taifa ya Ureno, Andre Silva.

Silva amekua katika kiwango kizuri katika klabu ya Porto msimu huu huku tayari akiwa ametupia magoli 15. Gazeti moja la Ureno liitwalo A Bola limedai Ronaldo amezungumza na uongozi wa Bernabeu kumnasa mkali huyo.

Hapa chini ni stori nyingine za usajili zilizobamba magazeti ya Ulaya leo Jumatano,


  • Chelsea wana imani kubwa ya kumnasa Romelu Lukaku majira ya joto ambapo mshambuliaji huyo akionya kwamba hataongeza mkataba mwingine na klabu yake ya sasa Everton.

  • Kinda kutoka klabu ya Marseille ya Ufaransa,  Maxime Lopez amefunguka kwamba Liverpool walimfata mwaka jana huku akidai anaweza kua mbadala wa Philippe Coutinho.

  • Arsenal wameripotiwa kua katika mipango ya kukuamilisha dili ya kumsajili beki wa Eibar, Florian Lejeune majira haya ya joto.

  • Kocha anayetazamwa kwa karibu na klabu ya Barcelona, Ernesto Valverde wa Athletic Bilbao anatarajiwa kufanya maamuzi kuhusu hatima yake wiki hii.

  • NewCastle wanatizamia kumsajili beki kutoka St. Etienne, Mikael Nade na wa Nice,  Wylan Cyprien.
Ronaldo ampigia debe Mreno mwenzake Real Madrid, Chelsea bado wanamtaka Lukaku, hizi hapa stori za usajili magazeti ya Ulaya leo Ronaldo ampigia debe Mreno mwenzake Real Madrid, Chelsea bado wanamtaka Lukaku, hizi hapa stori za usajili magazeti ya Ulaya leo Reviewed by Steve on Wednesday, March 15, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.