Conte afurahishwa na ushindi dhidi ya Man United, aizungumzia kadi ya Herrera
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amefunguka kwamba amefurahishwa na kikosi chake kufanikiwa kusonga hatua ya nusu fainali katika kombe la FA baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United usiku wa jana.
N'Golo Kante ndiye mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo uliopigwa ndani ya dimba la Stamford Bridge ambapo sasa Chelsea watakutana na Tottenham katika nusu fainali uwanja wa Wembley.
Man Unite walijikuta wakicheza 10 pekee uwanjani baada ya Ander Herrera kutolewa kwa kadi ya pili ya njano kufuatia rafu aliyomchezea Eden Hazard.
"Ulikuwa ni mchezo mzuri dhidi ya kikosi imara chenye wachezaji wazuri. United wana kikosi kizuri katika ligi. Kwetu ni furaha kwenda hatua nyingine." aliwaambia waandishi.
Kuhusu kadi nyekundu ya Herrera, Conte amefunguka kwamba "Nadhani Hazard alianza mchezo na alishindwa kucheza. Watu wote waliona na wanaweza kuhukumu."
Chelsea sasa wamefikisha michezo 12 ya hivi karibuni bila kushindwa mbele ya Manchester United katika mashindano yote.
Conte afurahishwa na ushindi dhidi ya Man United, aizungumzia kadi ya Herrera
Reviewed by Steve
on
Tuesday, March 14, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment