Kaburu akubali kuwaunga mkono Yanga kimataifa, lakini kuhusu ubingwa kawaambia hivii..
Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu', amesema wanawaunga mkono wapinzani wao Yanga katika harakati zao za kimataifa lakini amewataka wasijisumbue kuhusu ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa hata iweje lazima wabebe.
Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Zanaco ya Zambia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo kwa kiasi fulani yameiweka njiapanda Yanga kwani sasa italazimika kusaka ushindi katika mchezo wa marudiano utakaochezwa wikiendi hii jijini Lusaka ili iweze kusonga mbele hatua inayofuata.
Kaburu amesema wanawaombea Yanga kila la heri katika mashindano ya kimataifa kwa kuwa wanaiwakilisha Tanzania hivyo wataendelea kuwasapoti kwa kila namna.
"Si Yanga tu hata Azam mechi za kimataifa wanazocheza si kwa ajili ya timu zao ila wanaiwakilisha Tanzania hivyo hatuna budi kuungana nao na kuwatakia heri kwenye michezo yao.
"Lakini licha ya kuwatakia heri, wanapaswa kufahamu kwa ligi ya nyumbani hawana chao wakirudi jambo wanalotakiwa kulijua ubingwa lazima uende Msimbazi," alisema.
Kaburu akubali kuwaunga mkono Yanga kimataifa, lakini kuhusu ubingwa kawaambia hivii..
Reviewed by Steve
on
Tuesday, March 14, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment