Propellerads

Uteuzi wa Hassan Kessy Taifa Stars watia shaka kwa kushindwa kukidhi mambo kadhaa, lakini kocha Mayanga amkingia kifua




Uteuzi wa beki wa Yanga, Hassan Kessy katika kikosi cha Taifa Stars umeibua mjadala mkubwa kutokana na idadi ndogo ya mechi alizocheza staa huyo msimu huu lakini kocha wa muda wa timu hiyo, Salum Mayanga amemtetea.

Kessy alicheza mechi tano katika duru la kwanza la ligi kuu bara kabla ya kupewa nafasi katika mechi nne za hivi karibuni. Hii inamaanisha beki huyo wa kulia amecheza mechi zisizofikia asilimia 50 msimu huu jambo limetia doa uteuzi wake.

"Nimempa nafasi Kessy (Hassan) kutokana na mfumo wangu. Mara nyingi napendelea kutumia mfumo wa 4-4-2 hivyo Kessy anamudu vizuri katika aina hiyo, kama atashindwa kufikia malengo yangu nitafanya mabadiliko."

"Tutaingia kambini Machi 19 na tutacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Botswana na Burundi, baada ya hapo nitakuwa nimepata picha halisi ya kikosi," alieleza.
Uteuzi wa Hassan Kessy Taifa Stars watia shaka kwa kushindwa kukidhi mambo kadhaa, lakini kocha Mayanga amkingia kifua Uteuzi wa Hassan Kessy Taifa Stars watia shaka kwa kushindwa kukidhi mambo kadhaa, lakini kocha Mayanga amkingia kifua Reviewed by Steve on Tuesday, March 14, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.