Wanaodai mechi za Simba ni za mchangani, Luizio awapa neno
Mechi ya kirafiki kati ya Simba na Polisi Dodoma imechukuliwa kama haina mantiki yoyote na wenzao Yanga, wakicheza mechi za kimataifa na Zanaco, lakini straika wa timu hiyo, Juma Luizio ameweka wazi kwamba inawajenga.
Luizio alifafanua kwamba Polisi Dodoma ni timu ndogo haiwezi kulinganishwa na hadhi ya Simba, ila alisema ina wachezaji ambao wana kiu ya kuonekana na kuonyesha umahiri mbele ya mastaa ambao wanawasikia kwenye vyombo vya habari.
"Ni kweli kwenye soka hapakosekani kejeli, unajua siku tuliyocheza na Yanga walicheza mechi ya kimataifa na Zanaco ambayo ni timu bora hivyo sisi kucheza na Polisi Dodoma ikaonekana kama hatuna jipya ila ifahamike kwamba huku ndiko kwenye soka la ushindani," alisema.
Luizio alisema timu za madaraja ya chini zina kiu ya kupanda ama kuonekana na wadau hivyo zinapopata bahati za kucheza na timu zilizo na majina, wachezaji wanajituma kuliko inavyodhaniwa.
"Unafikiri nini kama watu walikuwa wanamsikia Mavugo, Kichuya ama mchezaji yoyote kwenye vyombo vya habari halafu ikatokea nafasi ya kucheza nao, lazima watajituma ili kuonyesha uwezo wao na pengine kuonekana na viongozi ili waweze kusajiliwa," alisema.
Wanaodai mechi za Simba ni za mchangani, Luizio awapa neno
Reviewed by Steve
on
Tuesday, March 14, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment