Busungu afafanua kuhusu hatima yake na klabu ya Yanga
Imefahamika kuwa Mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu tayari ameonyeshwa mlango wa kutokea baada ya yeye mwenyewe kukiri hilo kwa kusema anaona kila dalili za kutothaminiwa.
Busungu aliyejiunga na Yanga akitokea Mgambo JKT ya Tanga misimu miwili nyuma, amekosa nafasi ya uhakika katika kikosi cha Yanga, Jumapili iliyopita alipata bahati ya kucheza mechi ya Ligi kuu Bara dhidi ya Mtibwa ambapo matokeo yalikua suluhu.
Mshambuliaji huyo ana wakati mgumu mbele ya wapinzani wake Amissi Tambwe, Donald Ngoma pamoja na Obrey Chirwa ambao wanaanza kikosi cha kwanza cha Yanga mara kwa mara.
Kumekuwa na taarifa nyingi kwamba Busungu ni miongoni mwa wachezaji wasiopendwa kikosini hapo na benchi la ufundi chini ya kocha George Lwandamina.
Busungu mwenyewe alipotafutwa alikua na haya ya kusema, "Ndugu yangu kuna mambo mengi yanafanyika lakini siwezi kuyasema, lakini ukiwa una akili timamu basi utakuwa unajua hasa nini kimelengwa kwako.
"Kwa sasa nilikuwa na matatizo yangu kibao yakiwemo ya kifamilia, ila ijulikane tu kuwa bado nipo Yanga na nikitakiwa kwenda mazoezini nitaenda bila ya matatizo, kuna msemo unasema mwenye macho hawaambiwi tazama, ndiyo hiyo inanitokea mimi kwa sasa hali yangu siielewielewi,"
Busungu afafanua kuhusu hatima yake na klabu ya Yanga
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 16, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment