Propellerads

Hii ndiyo klabu ya ligi kuu bara iliyo katika mazungumzo na Pluijm




Siku chache baada ya Yanga kutangaza kuachana na Mkurugenzi wake wa Ufundi, Hans Pluijm, jina la kocha huyo limechomoza katika timu ya Singida United.

Pluijm alivunjiwa mkataba na Yanga kwa madai kuwa wana tatizo la kiuchumi na alikuwa akisubiri kulipwa madai yake ili aondoke nchini.

Kwa sasa kumeibuka taarifa mpya, ambapo jina la kocha huyo Mholanzi kuchomoza Singida United, akitajwa kutakiwa kwenda kuimarisha benchi la ufundi linaloongozwa na Fred Minziro.

"Mazungumzo ya awali yamefanyika, kuna wadau wetu wapo Dar es Salaam wanatusaidia jambo hili la Pluijm.

"Tunaamini ni mtu sahihi akisaidiana na Minziro wataipa hadhi Singida United," kilisema chanzo cha taarifa na kukataa kusema kama Pluijm atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi au kocha zaidi ya kusisitiza ataibukia Singida United.


Hii ndiyo klabu ya ligi kuu bara iliyo katika mazungumzo na Pluijm Hii ndiyo klabu ya ligi kuu bara iliyo katika mazungumzo na Pluijm Reviewed by Steve on Thursday, March 16, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.