Kuhusu mikakati ya Ubingwa, Omog atoa onyo kwa wachezaji kikosini
Kocha wa Simba Joseph Omog, amesema hatokuwa na mzaha kwa mchezaji wake yeyote atakayefanya makosa na kusababisha wapoteze mchezo wowote iwe wa michuano ya Ligi Kuu au Kombe la FA.
Simba ipo nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara, lakini pia Jumapili wiki hii itacheza Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Madini FC ya Arusha.
Omog amesema hiki ni kipindi ni kipindi muhimu kwa timu hiyo, hivyo kila mchezaji anapaswa kuongeza umakini.
"Ukweli sitakuwa na mzaha kwa mchezaji yeyote atakayefanya kosa ambalo linaweza kutupotezea malengo yetu, nipo tayari kumkata mshahara au hata kumuondoa kikosini asicheze," alisema Omog.
Kocha huyo raia wa Cameroon, alisema katika mechi sita zilizosalia kwenye Ligi Kuu, angependa kuona kila mchezaji wake akicheza kwa kujitoa zaidi.
Alisema anatambua kila mchezaji kwenye kikosi chake ameonesha kuwa na kiu ya kuhakikisha wanapata mafanikio hayo, msimu hivyo hakuna tatizo litakalojitokeza na anaamini ndoto zao za kutwaa mataji yote mawili zina asilimia kubwa kufanikiwa.
Kuhusu mikakati ya Ubingwa, Omog atoa onyo kwa wachezaji kikosini
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 16, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment