Msuva aweka wazi mipango yake ya baadaye pindi tu akiondoka Yanga
Mchezaji wa Yanga, SImon Msuva amesema nguvu kubwa anayotumia katika timu yake hivi sasa, anategemea kuitumia pia katika timu mpya atakayoenda kucheza baada ya kumaliza mkataba wake Yanga.
Msuva amesema kuwa hatarajii kucheza Yanga milele, kwani ana malengo ya kusonga mbele zaidi.
Amefunguka kikubwa kwa sasa ana mkataba na Yanga wa mwaka mmoja anahitaji kuendelea kujitoa kwa nguvu kuisaidia timu ili atakapopata nafasi kwenye timu nyingine baada ya mkataba kuisha mambo yaendelee kuwa mazuri zaidi.
"Nguvu ninayoonesha leo hata nikiondoka Yanga na kucheza timu nyingine nitaendelea kuionesha kwa sababu kama mchezaji nina malengo makubwa mbele," alisema.
Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa wa zamani wa Mtibwa, alisema hawezi kuweka wazi anatarajia kwenda wapi, anaheshimu mkataba wake na timu anayochezea.
Msuva aweka wazi mipango yake ya baadaye pindi tu akiondoka Yanga
Reviewed by Steve
on
Thursday, March 16, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment