Man United kuwanasa hawa wawili kutoka Monaco, Terry kupigwa chini Chelsea!?...hizi hapa tetesi za usajili magazeti ya Ulaya leo
Manchester United wanajipanga kukamilisha uhamisho wa wachezaji wawili mkupuo kutoka Monaco, Kylian Mbappe na Tiemoue Bakayoko baada ya kukunwa na viwango vyao katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Imeripotiwa na ESPN kwamba wawakilishi wa Man United walihudhuria kwenye mechi kati ya Monaco na Man City dimba la Stade Louis II ambapo ilishuhudiwa wachezaji hao kila mmoja akifunga kwenye mchezo huo.
Stori nyingine kubwa kutoka magazeti ya Ulaya kuhusu usajili leo
- Itawabidi Chelsea kumpa mkataba utakaokua na thamani ya pauni 200,000 kwa wiki mlinda mlango Thibaut Courtois ili kuepuka harakati za Real Madrid kumnasa.
- Nyota wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amekataa ofa ya kurejea kucheza ligi ta Italia, Serie A katika klabu ya Napoli.
- Pep Guardiola anatizamiwa kutumia kiasi cha pauni mil 200 majira ya joto kukisuka kikosi chake baada ya kujikuta wakitolewa katika Champions League.
- Bosi wa Everton, Ronald Koeman ameonya kwamba Ross Barkley atauzwa mwishoni mwa msimu.
- Tottenham wapo katika mipango ya kukamilisha uhamisho wa Barkley na winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha.
- Arsenal na Tottenham Spurs ni miongoni mwa vilabu vinavyomfukuzia beki wa Eiber, Florian Lejeune.
- John Terry hatapewa mkataba mpya tena Chelsea majira ya joto, lakini anaweza kupewa majukumu ya ukocha.
Man United kuwanasa hawa wawili kutoka Monaco, Terry kupigwa chini Chelsea!?...hizi hapa tetesi za usajili magazeti ya Ulaya leo
Reviewed by Steve
on
Friday, March 17, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment