Propellerads

Hanspope ameamua kulifikisha hapa swala la Kessy



Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hanspope ameonekana kukomaa na beki wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Ramadhan 'Kessy', baada ya kusema wanasubiri fedha zao za malipo kutoka Yanga.

Simba wanatakiwa kulipwa Sh milioni 50 na faini ya Sh milioni tatu kutokana na Yanga kumsajili Kessy akiwa bado ana mkataba na Wekundu wa Msimbazi.

Yanga waliamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuilipa Simba kutokana na kesi iliyofungwa na kamati hiyo.

Hanspope amesema hawajui kilichokwamisha kulipwa fedha zao baada ya uamuzi wa kamati hiyo.

"Kamati ilishatoa uamuzi, hivyo sijui nini kinakwamisha wakati tulipaswa kulipwa fedha zetu," alisema.
Hanspope ameamua kulifikisha hapa swala la Kessy Hanspope ameamua kulifikisha hapa swala la Kessy Reviewed by Steve on Friday, March 17, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.