Nje ndani ya mkataba wa Pluijm na Singida United, Mwigulu Nchemba afunguka mpango mzima
Kocha mkuu wa zamani wa Yanga, Hans Van Pluijm, leo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Singida United iliyorejea Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amesema wameamua kumpa mkataba huo kutokana na kuridhishwa na uwezo wake.
Mwigulu ambaye pia ni waziri wa Mmbo ya Ndani, alisema kocha huyo atasaini mkataba huo ili kuipa mafanikio timu hiyo.
"Ni kweli Pluijm ametua Singida United, tutakuwa naye kwa miaka miwili na tutasaini naye mkataba kesho (leo) ili aisaidie timu yetu," alisema.
Kwa namna hiyo, kocha mzawa Fred Minziro atakuwa msaidizi wa Pluijm.
"Minziro hatuwezi kuachana naye, ataendelea kuwa na sisi ila pia leo (jana) tumemtambulisha mchezaji wa kigeni, nitakutajia jina lake," alisema Mwigulu.
Nje ndani ya mkataba wa Pluijm na Singida United, Mwigulu Nchemba afunguka mpango mzima
Reviewed by Steve
on
Friday, March 17, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment