Yanga wakiwa Zambia, Tambwe asalia Dar huku akifunguka juu ya hali yake
Kikosi cha Yanga kipo Zambia kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Zanaco FC, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka lakini huku nyuma Amissi Tambwe ni mmoja wa wachezaji waliobaki Dar.
Mshambuliaji huyo ambaye ni majeruhi akisumbuliwa goti, amesema kuukosa mchezo huo kwake ni pigo na ameumia kwa kiwango cha juu.
"Unajua soka ndio kazi yangu, kitendo cha kuwa nje ya uwanja nikipitwa na mechi muhimu kama hizo, zote mbili za Zanaco zimenipita, nimeumia sana na kuona kama vile sijaitendea haki klabu yangu," alisema Tambwe na kuongeza:
"Nilikuwa nimejipanga kufanya kweli ngazi ya kimataifa, lakini ndiyo hivyo sina jinsi. Nawaombea wenzangu kwa Mungu waliosafiri na timu wakapambane kwa nguvu zao zote na ni matumaini yangu kuwa wakifanya hivyo tutaibuka na ushindi kwani Zanaco hawatishi sana."
Yanga wakiwa Zambia, Tambwe asalia Dar huku akifunguka juu ya hali yake
Reviewed by Steve
on
Friday, March 17, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment