Mipango ya matibabu ya Ngoma na Tambwe, kitu 'spesho' kufanyika ili wapone haraka
Katika kuhakikisha wachezaji wao wanapona kwa haraka na kurejea uwanjani kuisaidia timu yao, viongozi na mashabiki wa Yanga wameanza mchakato wa matibabu kwa wachezaji Donald Ngoma na Amissi Tambwe.
Wachezaji hao hawakuwamo kwenye msafara wa timu hiyo uliokwenda Lusaka, Zambia juzi Alhamisi kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Zanaco.
Ngoma yupo nje kutokana na maumivu ya nyama za paja aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Zanaco wakati awali alikuwa na majeraha ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja kwa wiki tatu pamoja na Tambwe ambaye inadaiwa goti lake limejaa maji.
Kwa taarifa za chini kwa chini zilizopatikana zinadai kwa viongozi na mashabiki wa timu hiyo wamepanga kuwapeleka wachezaji hao nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya haraka.
"Tunafahamu kabisa kuwa Ngoma na Tambwe mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu, lakini siyo sababu kwetu sisi tushindwe kuwatibia.
"Kwa sababu wachezaji hao walipata majeraha hayo wakiwa wanaichezea Yanga, hivyo hatuoni sababu ya kutowatibia na kingine tunaamini ni kama fundisho kwa wachezaji wengine wenye mikataba ya kuendelea kuichezea Yanga kama ilivyo kwa akina Ngoma na Tambwe, kikubwa tunataka kujenga uaminifu na moyo wa kuipambanua timu yao.
"Hivyo tumepanga kuwapeleka Sauzi kwani ndiyo nchi ya kwanza tuliyoipendekeza hadi hivi sasa na kikubwa tunataka kuona wachezaji hao wanapatiwa matibabu ya haraka na wanarejea uwanjani wakiwa na nguvu tele," kilieleza chanzo cha taarifa.
Mipango ya matibabu ya Ngoma na Tambwe, kitu 'spesho' kufanyika ili wapone haraka
Reviewed by Steve
on
Saturday, March 18, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment