Propellerads

Ile ishu ya udhamini wa Sportspesa kwa Yanga imefikia hatua hii....




Kampuni ya kuendesha michezo ya kubahatisha ya Sportspesa yenye makao makuu yake Kenya imeahidi kuwa kama makubaliano yakienda vizuri na kusaini mkataba wa kuidhamini Yanga, basi tatizo la ukata wanalokabiliana nalo litamalizika.

Hii inaweza ikawa ni habari njema kwa kwa viongozi na mashabiki wa Yanga baada ya kuwepo kwa taarifa za kufikia makubaliano mazuri ya mkataba ya udhamini wa timu hiyo.

Sportspesa inaidhamini klabu kubwa ya Hully City inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza, nyingine ni Kenya Rugby Union ( Sh 607 milioni), Kenyan Premier League (sh 450 milioni), Gor Mahia (sh 325 milioni) na AFC Leopards (sh 225 milioni).

Kwa taarifa zilizopatikana kutoka mitandao ya nchini ya Kenya, mazungumzo yanakwenda vizuri na Yanga na kilichobakia ni kusainishana mkataba na kampuni hiyo kuanza kazi.

"Ninaamini kabisa udhamini wa Sportspesa utamaliza tatizo la kiuchumi walilonalo Yanga hivi sasa na kurejea katika hali yao.

"Tunashukuru mazungumzo yetu yanaendelea vizuri na Yanga na wakati wowote tutafikia makubaliano mazuri na kusainiana mkataba, tunaamini ni klabu kubwa itakayoweza kututangaza kimataifa," alifunguka mtoa taarifa ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi.
Ile ishu ya udhamini wa Sportspesa kwa Yanga imefikia hatua hii.... Ile ishu ya udhamini wa Sportspesa kwa Yanga imefikia hatua hii.... Reviewed by Steve on Saturday, March 18, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.