Propellerads

Suala la ufungaji bora, Kichuya hana kinyongo akichukua yeyote ila isipokuwa wachezaji hawa




Shiza Kichuya ambaye yupo nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora msimu huu kwenye ligi kuu akiwa nayo 11, amesema kama akikosa nafasi ya yeye kuwa mfungaji bora basi angependa kuona Simon Msuva wa Yanga mwenye 12 akichukua kiatu hicho na siyo mchezaji kutoka nje ya nchi.

Baadhi ya wachezaji ambao wapo kwenye mbio za kuwania kiatu hicho na Amissi Tambwe mwenye tisa, Donald Ngoma ana  mabao nane akiwa sawa na Obrey Chirwa, wachezaji wote hawa wanachezea Yanga.

Kichuya amesema kwa jinsi ushindani ulivyo sasa katika kuwania ufungaji bora kwa upande wake yupo radhi kiatu hicho kikatua kwa mpinzani wake ama mtu yeyote lakini hatafurahi akiona kinaenda kwa mchezaji kutoka nje ya nchi.

"Mimi nimeshasema tangu mwanzo atakayechukua kiatu ndiye aliyepangiwa na Mungu, ila naomba achukue wa hapa kwetu yeyote kati yetu na hata akichukua Msuva ni sawa tu.

"nimejipanga kuhakikisha naisaidia timu yangu iweze kutwaa ubingwa msimu huu kwa kuhakikisha najituma mazoezini na kuifanya timu iweze kua vizuri zaidi na kuweza kufunga, iwapo nitafanikiwa kufunga na kuchukua kiatu itakuwa sawa, kuhusu kufanikiwa kufunga Yanga mara mbili kwenye ligi msimu huu ni kutokana na kujituma tu mazoezini na hakuna siri yoyote," alisema Kichuya.
Suala la ufungaji bora, Kichuya hana kinyongo akichukua yeyote ila isipokuwa wachezaji hawa Suala la ufungaji bora, Kichuya hana kinyongo akichukua yeyote ila isipokuwa wachezaji hawa Reviewed by Steve on Saturday, March 18, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.